Wenyeji wa fainali za mataifa ya Amerika ya kusini (Copa America) timu ya taifa ya Chile wamefanikiwa kutinga katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Chile.

Mchezo huo uliounguruma usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa taifa (Estadio Nacional) uliopo mjini Santiago ulishuhudia mabao ya ushindi ya wenyeji yakipachikwa wavuni na mshambuliaji wa klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli ya nchini Italia, Eduardo Jesús Vargas Rojas katika dakika ya 42 na 64.
Bao la kujipoza na machungu ya kupoteza mchezo huo wa hatua ya nusu fainali kwa upande wa Peru lilifungwa na Gary Medel dakika ya 60, baada ya kujifunga mwenyewe kufuatia hitilafu ya mawasilino na mlinda mlango wake Claudio Andrés Bravo Muñoz.

Hata hivyo kikosi cha Peru kilimaliza mchezo kikiwa pungufu baada beki wa klabu ya Eintracht Frankfurt ya nchini Ujerumani Carlos Zambrano kuonyeshwa kadi nyekundi kufuatia rafu mbaya aliyomcheza Charles Aranguiz.

Kufuatia ushindi huo, wenyeji Chile wanamsubiri mshindi wa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ambao utachezwa usiku wa hii leo kati ya Argentina na Paraguay kwenye uwanja wa Municipal de Concepción, uliopo mjini Concepción.

Chelsea Wamsaka Mziba Pengo La Cech
Picha: Ali Kiba Apangiwa Staa wa Kike Ndani ya Coke Studio Africa
Tags