China imetangaza ushuru wenye thamani ya dola bilioni 50 kwa bidhaa kutoka Marekani, ikilipiza kisasi cha ongezeko jipya la ushuru lililotangazwa na Marekani.

Orodha hiyo iliyotangazwa na China inajumuisha asililimia 25 ya ushuru wa forodha kwa aina 659 ya bidhaa zikiwemo za kilimo, magari na majini.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya China ambayo, hata hivyo, haikufafanua zaidi kuhusu bidhaa zilizoongezewa ushuru.

“China haitaki kupigana kwenye vita vya kibiashara, lakini kwa kukabiliwa huku na ukosefu wa kuona mbali wa  Marekani, China inalazimika kulipiza vikali,”imesema taarifa hiyo

Hata hivyo, uamuzi huo wa China unafuatia mara baada ya Marekani kutangaza ongezeko la ushuru wa dola bilioni 34 kwa bidhaa kutoka China na mipango ya kutangaza nyengine bilioni 16 kwa bidhaa nyenginezo hapo baadaye.

 

Ommy Dimpoz anusurika kifo, 'nimefanyiwa oparesheni'
Rais Kenyatta afuata nyayo za JPM