Baada ya kuzuka kwa virusi vya Corona nchini China, mji wa Wuhan unaharakisha kujenga Hospitali mpya kusaidia kutibu Wagonjwa waliokumbwa na Virusi hivyo ambavyo vimeua watu 80 na zaidi ya 870 wameambukizwa.
Madaktari nchini humo wamesema Waathirika wanapanga foleni kwa muda mefu wakiwa wanasubiri huduma kutokana na kusambaa kwa virusi hivyo.
Hata hivyo baadhi ya madaktari wameambiwa wasiende kutoa huduma kutokana na uchache wa vifaa vya kujilinda ili wasipate maambukizi.
Hata hivyo mamlaka katika Mji wa Wuhan zimesema hospitali hiyo inatarajiwa kuwa na uwezo wa kuwekwa vitanda 1000 vya wagonjwa na inatarajiwa kuanza kutumika Februari 03.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2003, Beijing ilijenga Hospitali ya Xiaotangshan ndani ya siku 7 iliyosaidia kutibu wagonjwa waliogua SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome), ugonjwa ulisababishwa na Virusi na kuua takriban watu 774 Duniani kwa mwaka 2002 na 2003.