Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya China, Wang Yi anatarajiwa kutua nchini kesho Januari 7 2021, katika uwanja wa ndege wa Chato na kufanya mazungumzo binafsi na Rais John Magufuli kisha kufanya mazungumzo rasmi ya kiserikali.

Wang anatarajiwa kuzindua chuo cha ufundi wilayani Chato na kutembelea mwalo wa ziwa Victoria wilayani humo kuangalia shughuli za uvuvi.

Aidha, atashuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa awamu ya tano ya reli ya kisasa (SGR) inayotoka Mwanza hadi Isaka yenye urefu wa kilometa 341. 

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chato Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema awamu hiyo ya ujenzi itagharimiwa na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Sh3.0617 trillioni na itajengwa na kampuni mbili kutoka China. 

Waziri Wang yupo kwenye ziara ya siku tano katika bara la Afrika ambapo kwa Tanzania atakuwepo kwa siku mbili akishiriki mazungumzo binafsi na Rais John Magufuli kisha kufanya mazungumzo rasmi ya kiserikali ya yeye na ujumbe wake.

Serikali yatangaza ajira 5000 za walimu

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 7, 2021
Serikali yatangaza ajira 5000 za walimu

Comments

comments