Serikali ya China imetangaza kuwaruhusu Wananchi wake kuongeza idadi ya watoto wanaopaswa kuzaliwa katika familia moja.

Mapema leo, Shirika la Habari la China liliripoti kuwa chama cha Kikomunisti cha China kitalegeza msimamo na kuwakubalia Wapenzi/Wanandoa kuzaa Watoto watatu badala ya wawili kutokana na idadi ya Wazee kuongezeka nchini humo.

Tangazo hilo linafuatia takwimu za sensa zilizoonesha kuwa idadi ya Wachina walio katika umri wa kufanya kazi imepungua katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita huku idadi ya Watu walio na zaidi ya umri wa miaka 65 ikiwa imeongezeka.

Jambo hili limewekea shinikizo dhidi ya uchumi na jamii, Chama hicho Tawala cha China kiliweka vikwazo vya idadi ya Watoto kwa wazazi tangu 1980 ili kudhibiti idadi ya Watu nchini humo.

Mwaka 2015 vikwazo vya Wazazi kuwa na Mtoto mmoja viliondolewa na idadi hiyo ikaongezwa na Wazazi.

Nyota wa zamani wa Liverpool, PSG atua Tanzania
Mwakinyo: Huyu sio bondia mwenyewe