Jopo wataalamu kutoka shirika la Afya Duniani (WHO), baada ya kufanya ukaguzi nchini China kwa siku 9 kwa kuangalia hatua zilizochukuliwa na nchi hiyo katika kupambana na Corona wametoa takwimu kwa umma.
Kwa wiki mbili zilizopita kila siku wagonjwa wapya zaidi 2,000 waliripotiwa, mara baada ya wataalamu hao kumaliza kazi yao, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa jana ilikuwa 416, ambayo imepungua kwa asilimia 80 ndani ya wiki 2.
Mshauri Mwandamizi wa Katibu Mkuu wa WHO, Bruce Aylward amesema tathmini ya kundi hilo imeona hatua zinazochukuliwa na China kuhamasisha Serikali na watu wote katika jamii kupambana na maambukizi ya virusi hiyo, zimezuia maelfu ya wagonjwa wapya kutokea, na hayo ni mafanikio makubwa.
Kundi hilo pia limependekeza nchi mbalimbali kufanya kazi ya usimamizi na ukaguzi, ili kuwagundua, kuwathibitisha, kuwaweka karantini na kuwatibu mapema wagonjwa wa virusi vya Corona.