Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally amemuhakikishia mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara gavana wa jimbo la Fujian nchini China na kumsihi kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja na Tanzania katika maeneo hayo.
Katibu Mkuu Dkt. Bashiru ameyasema hayo alipokutana na kiongozi huyo na kumuomba jimbo lake kushirikiana na Tanzania katika sekta ya biashara, utalii na utafiti ambapo jimbo hilo tayari linatoa udhamini wa masomo kwa baadhi ya watanzania.
Amesema Rais Dkt. John Magufuli ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini China mwakani, atamshawishi kutembelea Fujian kutokana na kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni na mpangilio mzuri wa ardhi na utunzaji wa Mazingira.
Katibu mkuu Dkt. Bashiru anaongoza ujumbe wa watanzania takribani 20 makada wa chama cha Mapinduzi kwenye ziara ya kimafunzo kwa mwaliko wa chama cha kikomunisti cha China, CPC.