China imeiomba Marekani iachane na fikra ya ‘Vita vya baridi’ baada ya Washington kusema inapanga kupanua mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia kwa kuunda mabomu madogo.
Jeshi la Marekani limesema kuwa silaha zake za nyuklia zinaonekana kuwa kubwa kustahili kutumika na sasa inataka kutengeneza mabomu madogo madogo.
“Nchi inayomiliki silaha kubwa za nyuklia duniani, inapaswa kuongoza mkondo badala ya kwenda kinyume ,” Waziri wa ulinzni wa China alisema Jumapili.
Aidha, Marekani ina wasiwasi na silaha zake za nyuklia kuwa hazitoweza kutumika tena, na hazina tishio. pia Imeitaja Uchina, Urusi Korea kaskazini na Iran kama mataifa yanayoweza kuwa tishio kwake kuachana na mpango wake wa nyuklia.
Hata hivyo, Nyaraka iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani siku ya Ijumaa- inayojulikana kama Nuclear Posture Review (NPR), inadai kuwa kutengeneza silaha ndogo za nyuklia itasaidia kupambana na fikra kuwa Marekani sio tishio. Silaha hizo ndogo hazina nguvu sana lakini bado zinaweza kusababisha madhara.