China imeanza rasmi juhudi ya kuzipatanisha nchi za Pakistan na Afghanistan mara baada ya kutokea kwa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka miwili.
Aidha, nchi hizo zinatuhumiana kila upande kuwa mmoja wao anasaidia magaidi ambao wamekuwa wakishambulia nchi hizo na kuhatarisha usalama wa eneo hilo.
China imejitosa katika upatanishi wa nchi hizo mara baada ya Serikali ya Afghanistan kupendekeza kuwepo nchi nyingine ya kati itakayyosimamia mazungumzo hayo ya kutafuta amani.
Hata hivyo, pande zote mbili Afghanistan na Pakistan zimekutana na kufanya mazungumzo kuhusu suala la ushirikiano kati ya nchi hizo na hali ya usalama wa eneo hilo.