Wakati sehemu kubwa ya watu nchi za Afrika ikiwa bado inatumia mfumo wa mawasiliano kwa kasi ya 3G na 4G, Wizara ya Sayansi na Teknolojia, China imezipa jukumu la kuendeleza mfumo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano ya simu wa 6G, ofisi zake mbili.

Wizara hiyo imebainisha kuwa moja ya Ofisi hizo inajumuisha Mawakala wa Serikali wanaowajibika katika utungaji wa sera husika na nyingine inajumuisha Wataalamu 37 watakaowashauri watunga Sera.

Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Wang Xi amesema ujuzi kuhusu teknolojia hiyo bado upo katika hatua za majaribio bila kuwepo kwa ufafanuzi wa makubaliano na matumizi yake.

Alisema, Wizara yake itafanya kazi na idara husika kuweka mpango wa maendeleo ya 6G, na itafanyia kazi mafanikio katika nadharia zake za msingi, teknolojia na viwango muhimu.

Samatta amchambua 'fundi aliyempikia' bao la kuifunga Liverpool
Wizi wa kura 2015 wamfikisha Msigwa kamati ya maadili