China imeripoti visa vipya 17 vya maambukizi ya corona ambapo 10 kati ya hivyo yakiwa ni maambukizi ya ndani huku wagonjwa watano wakiwa wanatokea mji wa Wuhan.

Visa hivyo vilivyotokea Wuhan ni vya kwanza katika kipindi cha takriban mwezi mzima na kuzua hofu kuwa huenda wimbi la pili la mlipuko wa covid 19 linaanza katika mji huo uliokuwa kitovu cha mlipuko duniani.

Imeelezwa kuwa mji wa Jilin umewekwa katika zuio la kutoka nje baada ya kuwa na visa 10 vilivyoripotiwa, Mei 10. Mamlaka hazijataja muda wa kuisha kwa zuio hilo.

Hadi sasa, China ina jumla ya visa 82,918 ambapo 780 ni wagonjwa walio chini ya uangalizi ambao bado hawajaanza kuonyesha dalili. Wagonjwa 78,144 wameripotiwa kupona huku kukiwa na jumla ya vifo 4,600.

Kisa cha mapenzi chimbuko la kampuni iliyotajirika na Corona
Video: Shehena sukari yatua, CHADEMA yafanya maamuzi magumu