China imethibitisha kuwa inamshikilia rais wa Interpol Meng Hongwei aliyepotea kwa ajili mahojiano.

Ikulu ya Beijing imesema kuwa alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria.

Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupotea baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa, kwenye makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25 mwaka huu.

Aidha, Interpol imesema kuwa imepokea mara kadhaa barua ya kutaka kujiuzulu kazi kutoka kwake lakini haijamruhusu.

Familia ya Meng haijawasiliana naye tangu aondoke katika makao makuu hayo ya Interpol nchini Ufaransa kitu ambacho kimezua hofu kubwa.

Pia Gazeti la South China Morning Post lilinukuu taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.

Hata hivyo, haijulikani ni kwani nini rais huyo wa Interpol alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu za China au alikofifichwa ni wapi.

 

Licha ya kuyumbisha jahazi, Guardiola ampongeza Mahrez
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 8, 2018