China imetangaza kuwa haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati kuitaka Bejing kufuata nyayo za Taiwan ambayo imeruhusu ndoa za jinsia moja.

Msemaji wa Bunge la China amesema kuwa msimamo wa kisheria wa China unabaki ule ule wa kutambua kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.

Aidha, mwezi Mei 2019 Taiwan ilikuwa taifa la kwanza la Asia kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja baada ya mjadala wa miaka mingi juu ya usawa wa ndoa.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuwa kuna jamii kubwa ya mashoga katika miji mikubwa ya China, ambapo katika miezi ya hivi karibuni jamii hiyo imekuwa ikilengwa kwa kuhesabiwa na kuzusha hofu huenda Wachina wakaanza kutowavumilia.

Bunge la Uganda lapinga hukumu ya kifo
Mwanaharakati ahukumiwa kwenda jela maisha