China imetoa onyo kali kwa Marekani kufuatia hatua yake ya kutuma meli ya kivita katika eneo la kisiwa chake kilichoko kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China, Yang Yujun ameeleza kuwa nchi yake itachukua hatua zote za lazima kuilinda nchi hiyo dhidi ya uchokozi wowote utakaofanywa na Marekani.

Marekani imekiri kuwa meli hiyo ya Kivita aina ya USS Curtis Wilbur, missile destroyer ni mali yake.
Msemaji huyo wa Wizara ya Ulinzi wa China ameitaja hatua hiyo ya Marekani kuwa haizingatii weledi wa kijeshi na ina taswira ya uzembe na kutishia usalama.

Alisema kuwa Marekanji imevunja sheria za China na kuingilia amani, usalama na mipaka ya maji kutishia amani na usalama wa eneo hilo, kitendo alichodai ni hatari kwa vikosi vya pande zote mbili.

 

Thamani Ya Usajili Yapanda Kwa Bilioni 1
Octopizzo apigilia tena msumari baada ya kuwaomba radhi Nameless na Wahu

Comments

comments