Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendeleza kila kitu kilichopangwa kufanyika, kutokana fedha anazotoa katika miradi kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo mradi wa umeme wa JNHPP (MW 2115), ujenzi wa Daraja wa Busisi, ununuzi wa ndege, madarasa, vituo vya afya na utalii.

Dkt. Biteko amesema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Bukombe mkoani Geita kwenye ziara ya kikazi aliyoianza, huku akiwataka Watendaji na watumishi nchini kusimamia matumizi sahihi ya fedha za Serikali, kwani ndizo zinategemewa kuwaletea maendeleo Watanzania.

Amesema, “Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassani hakuna hata kimoja kilichosimama iwe Bukombe, iwe Bogwe, iwe Nyang’wale iwe Chato, iwe Bochosa iwe Sengerema iwe Tandahimba, iwe Arusha na Mahali popote Tanzania kila kilichopangwa kinafanyika.”

Aidha, Naibu Waziri Mkuu Biteko amesema, Rais amewafanya Watanzania wawe daraja la juu kwa fedha anazowapatia kwa ajili ya maendeleo yao, ikiwemo Madarasa, Vituo vya Afya, Barabara, Maji na Miundombinu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya watu.

Walimu, Madaktari wapigwa marufuku kusimamia miradi
Waislamu wakutana kukumbushana maadili katika Dini