Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo ameuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kumsimamia mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kidatu – Ifakara, yenye urefu wa kilomita 65.9 Mkoani Morogoro, ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Awali akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Lazack Kyamba alimueleza Katibu Mkuu kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza Oktoba 2, 2017 kwa kipindi cha miezi 30 na ulipangwa kukamilika April 30, 2020, lakini ilishindikana kutokana na changamoto mbalimbali.
Amesema, hadi kufikia Desemba 31, 2022 utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 73.6 ikilinganishwa na mpango kazi wa asilimia 100.
Chongolo, yupo kwenye ziara ya kusimamia, kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu), na viongozi wa Chama na Serikali Mkoani Morogoro.