Chris Brown ameanza kupangua hoja za waendesha mashtaka kuhusu kesi ya kufuga nyani nyumbani kwake bila kibali husika.

Mwimbaji huyo aliingia kwenye matatizo na vyombo vya sheria baada ya video inayomuonesha mtoto wake wa kike, Royalty akiwa anacheza na nyani ambaye alitajwa kwa jina la Fiji, kusambaa mitandaoni Desemba mwaka jana.

Alifunguliwa kesi mahakamani ambapo kwa sheria za nchini humo, endapo atakutwa na hatia atafungwa jela kwa kipindi cha miezi sita.

Katika utetezi wake, mwimbaji huyo ameeleza kuwa hajawahi kufuga nyani nyumbani kwake Los Angeles kama ilivyoelezwa na waendesha mashtaka. Alieleza kuwa nyani aliyerekodiwa akiwa na mwanaye anamilikiwa na ndugu yake ambaye ana kibali.

Mtoto wa Chris Brown, Royalty akiwa na Fiji

Alielezea kuwa walikutana siku moja na ndugu yake huyo akiwa na Fiji na ndipo mwanaye Royalty alicheza naye na kuchukuliwa video hizo.

“Mimi sio Michael Jackson, sifugi nyani nyumbani kwangu,” alisema Chris Brown.

Hata hivyo, utetezi huo umepingwa na upande wa Serikali ambao wamemchukua Fiji na kumhifadhi katika jumba maalum la wanyama huko Los Angeles.

Kesi hiyo itasikilizwa February 6 mwakani.

Kikokotoo chamuibua tena Bulaya, 'Bora mjiuzulu'
Mzee wa kanisa atupwa jela maisha kwa kumbaka mtoto