Maisha aliyoyapitia Chris Brown hadi kuifanya dunia kuusikiliza muziki wake yamekuwa sehemu ya tiba iliyoyanusuru maisha ya shabiki aliyekuwa katika harakati za kujitoa roho.

Chris Brown ameamua kuweka wazi mkasa huo wa kunusuru maisha ya shabiki wake kupitia Instagram kwa kupost vipande vya jumbe walizokuwa wakijibishana kupitia mtandao huo (DM) usiku wa manane.

Post hizo zinaonesha kuwa shabiki huyo aliyemueleza Chris kuwa amekuwa akisumbuliwa kichwani na mawazo ya kutaka kujiua na kwamba anatafuta jinsi ya kuyazuia mawazo hayo. “Ukiwa kama mtu maarufu ninayemuangalia, nimefikiria tu kama utajibu ujumbe huu na kunipa matumaini,” aliandika shabiki huyo.

Ingawa Breezy anaweza kuwa bize sana na ziara yake kubwa ya ‘One Hell of a Nite’, alitumia muda wake kuusoma ujumbe huo na kumjibu kutoka moyoni maelezo ya kutosha yaliyobadili mawazo yake.

“Hilo haliwezi kuwa jibu. Kujiua sio kitu ambacho ninaweza kukaa nacho vizuri. Unafikiria kuchukua maamuzi kutokana na hisia zako. Maisha ni magumu sana katika baadhi ya nyakati lakini ni mazuri sana ukibaini mapema!”

“Niliwahi kuwa huko kiakili. Halafu nikawa na imani kwa Mungu (sio kwa binadamu/watu). Wote tumepotea na wote tunataka kusikia upendo, kukubalika na furaha! Nilipambana na nafsi yangu na shetani wangu kila siku! IMANI. Utajiri/Umasikini hauna maana. Kujishtukia na maoni ya watu inafunika mawazo yetu,” sehemu ya ushauri wa Chris kwa shabiki unasomeka.

Chis Brown

Sehemu ya jumbe kati ya Chris Brown na shabiki

Baada ya maelezo marefu ya kina, shabiki huyo aligubikwa na furaha na kumshukuru sana Breezy kwa kuponya maisha yake.

“Asante! Haujutu tu kiasi gani maneno hayo mema (kutoka kwa mtu kama wewe) yanamaana kwangu katika nyakati kama hizi. Saa 9 usiku, akili yangu ilikuwa inakimbia, nilikuwa na mawazo hasi na nilihitaji sana hiki,” alijibu Shabiki huyo.

Chris Brown aliwahi pia kukiri kuwa alishafikiria kujitoa roho baada ya kuachana na Rihanna.

Video: Rais Magufuli ametaka kodi yake ikatwe ili kuongeza mapato ya serikali.
Nuhu Mziwanda na tattoo mpya ya mrembo mwingine