Chris Brown amefanya tendo jema la kumfuta machozi mwanamke aliyefanyiwa unyanyasaji na mumewe kwa kumpa zawadi ya gari.

Zawadi ya Breezy ni sehemu ya sadaka yake ya Chrismas ambapo mbali na gari hilo la kifahari, amewapa zawadi ya midoli ya gharama watoto watatu wa mama huyo.

Zawadi ya Chris B

Akizungumzia uamuzi wake, mkali huyo wa ‘Loyal’ ameeleza kuwa awali alikuwa mchoyo, mkorofi na mwenye moyo mgumu lakini hivi sasa alipomuangalia machoni mwanamke huyo na watoto wake ambao kwa ujumla wao walinyanyaswa maisha yao yote, alijiona yeye.

Mwaka 2009, Chris Brown ambaye aliwahi kushambuliwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia na kumuumiza vibaya Rihanna ambaye alikuwa mpenzi wake.

“Najiona nipawaangalia hawa ndani ya macho. Kiasi cha ujasiri ambacho mama huyu amekuwa nacho ni cha ajabu. Natumaini ningeweza kuifanya sikukuu ya Christmas mwaka huu kuwa kubwa zaidi kwao,” alisema Chris Brown.

Kimbunga Cha Magufuli Chafyeka Maafisa Tanesco
Serikali Yawataka Wafanyakazi ‘Kuwasema’ Wakuu Wa Mikoa Wanaowaburuza Na Kuwatupa Selo