Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Christopher Maurice Brown maarufu Chris Brown anadaiwa kumbaka mwanamke kwenye boti iliyokuwa imeegeshwa nyumbani kwa Diddy Star Island.
Mwimbaji huyo anashtakiwa na Jane Doe ambaye ni mnenguaji/mtaalamu wa choreographer, mwanamitindo na msanii wa muziki, anaedai kwamba Chris alitoka kuwa rafiki wa kawaida hadi kuamua kumbaka, kwa dakika chache wakiwa ndani ya boti.
Kwa mujibu wa TMZ, mwanamke huyo anadai Chris Brown alimpigia simu na kumsihi aende nyumbani kwa Diddy kwenye Miami’s Star Island.
Alipofika huko mnamo Desemba 30, 2020, mwanamke huyo anadai Chris alimsogelea kwa ukaribu zaidi huku akimuuliza ikiwa alitaka kinywaji akimuelekeza kuelekea eneo la jikoni ndani ya boti hiyo walimokuwa
Jane Doe anadai aliingia jikoni na Chris brown, ambapo alimpa kikombe chekundu na kinywaji mchanganyiko na wakaanza kuongea na baada ya kujaza kikombe chake mara ya pili, anadai alianza kuhisi mabadiliko ya ghafla, yasiyoelezeka katika fahamu zake.
Akiendelea kuweka mambo wazi mwanamke huyo alidai kwamba alijihisi kuchanganyikiwa, kutokuwa sawa kimwili, na alianza kulegea na kujikuta kama mtu mwenye kunyemelewa na usingizi.
Anasema Chris alimwongoza chumbani kulala akiwa tayari amelewa na katika madai hayo, mwanamke huyo ameweka wazi kuwa Chris alifunga mlango wa chumba cha kulala, na kumzuia kujaribu kuondoka, akatoa nguo za ndani na kuanza kumbusu.
Anasema alinung’unika ili Chris Brown amuache, lakini aliendelea na kumbaka. Ingawa alikuwa amechanganyikiwa sana kwa wakati kiasi cha kutokujua afanye nini, anadai kwamba kwa sasa ameamua kumshtaki Chris akidai fidia ya dola milioni 20 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilion 46 za Kitanzania, akidai kuwa kitendo hicho kimemsababishia mfadhaiko wa kihisia.
Mawakili wa mwanamke huyo, Ariel Mitchell na George Vrabeck, wameweka bayana kuwa mteja wao hakuripoti madai ya ubakaji kwa polisi wakati huo kwa sababu alikuwa mwanafunzi hivyo alijaribu kuficha aibu yake.
Hadi sasa, hakuna chochote ambacho kimejibiwa na mwanamuziki huyo pamoja na uongozi wake.