Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido Adedeji Adeleke maarufu kama Davido amefunguka juu ya msanii nyota kutoka Marekani, Chris Brown kumsimamia kwenye harusi yake anayotarajia kufunga na mchumba wake Chioma ambaye siku chache zilizopita alimvalisha pete akiwa mwenye ujauzito wake.

Davido kupitia ukurasa wake wa Tweeter amesema kuwa msanii huyo nyota kutoka Marekani atakuwa mpambe wake (Best man) siku yake ya harusi ambayo anatarajia kufanya mwaka 2020.

“Chris amesema anataka kuwa mpambe wangu, hebu fikiria unamuona Chris kwenye vazi maalum la heshima, Chris amekubali kuwa mpambe wangu hebu vuta picha Chris yuko pembeni yangu” amesema Davido.

Aidha, Chris Brown amekuwa shabiki mkubwa sana wa nyimbo za Davido na mara kadhaa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amekuwa akijirekodi akisiiliza baadhi ya ngoma za Davido.

Hatua hiyo ilipelekea wawili hao kufanya ngoma ya pamoja inayoitwa ‘Blow mind’ ambayo ni moja ya ngoma nzuri kuwahi kufanyika kutoka kwa wasanii wakubwa Afrika na Ulaya.

Serikali kurasimisha ajira ya uvuvi
Philippe Coutinho afurahia maisha Allianz Arena