Chris Brown huenda akalazimika kuahirisha ziara yake ya muziki nchini Australia baada ya serikali ya nchi hiyo kuweka pendekezo la kumzuia kuingia nchini humo kwa madai ya tukio la kumpiga Rihanna mwaka 2009.

Waziri wa wanawake nchini Australia, Michaelia Cash alisema kuwa anaweza kuwasilisha pendekezo lake kwa waziri wa uhamiaji, Peter Dutton ili asimpe Visa Chris Brown.

“Watu wanapaswa kufahamu kuwa kama utafanya unyanyasaji wa wanawake halafu ukataka kusafiri kuizunguka dunia, kuna nchi ambazo zitakwambia ‘hauwezi kuingia kwa sababu wewe sio mtu mwenye tabia ambazo tungezitegemea nchini kwetu’,” alisema na kusisitiza kuwa Australia ni serikali ambayo haiogopi kusema hapana.

Chris Brown anategemea kuingia nchini Australia December mwaka huu kama ratiba ya ziara yake ya muziki iliyopewa jina la ‘One Hell of A Nite Tour’.

Mamia Ya Wahujaji Wafariki Kwa Kukanyangana Makka
Kikwete Azungumzia Kauli Za Magufuli Kuikosoa Serikali Yake