Baada ya kuwepo kwa taarifa za Meneja wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint- Germain ‘PSG’, Christopher Galtier kuwa kwenye hatari ya kutimuliwa kikosini hapo, mwenyewe ameibuka na kusema ataendelea kuipambania timu hiyo kuona inashinda taji msimu huu.
Galtier msimu huu ameshindwa kuivusha PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushuhudia timu yake ikiishia hatua ya 16 bora ikiondoshwa na mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich kwa jumla ya mabao 3-0.
Tayari aliyewahi kuwa Kocha wa Paris Saint-Germain, Thomas Tuchel anatajwa huenda akarejea kikosi hapo ambapo aliondoka mwaka 2021 baada ya kuifikisha timu hiyo fainali ya UEFA, Galtier ameanza kuinoa PSG msimu huu akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye alitumuliwa. Akizungumzia hali yake ndani ya
PSG, Galtier amesema: “Nimekuwa nikizungumza na uongozi kila wakati, Luis Campos (mshauri wa soka PSG) amekuwa upande wangu na hata rais naye amekuwa akinisapoti, malengo ni kumaliza msimu huu kwa kushinda taji.”
“Mimi kama kocha naendelea kupambana na kuipambania timu yangu kwa kuhakikisha inafanya vizuri.”
Katika Ligi ya Ufaransa PSG inaongoza msimamo wa Ligi hiyo ikiwa na alama 66 baada yakucheza michezo 27, ikifuatiwa na Olympic Marceilleyenye alama 56.