Kocha Mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino anaamini jeraha la Christopher Nkunku sio siriazi baada ya kuumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund.
Kocha huyo amesisitiza watafahamu zaidi kuhusu jeraha hilo baada ya kurejea London kwani alikazimika kutoka wakati mchezo ukiendelea katika Uwanja wa Soldier Field.
Pia, kocha huyo alidai mazingira mabovu ya uwanja haikuwa sababu ya straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuumia goti.
Imeelezwa sehemu ya Nkunku alipoumia ilikuwa ngumu kufuatia Tamasha la Mwanamuziki la Ed Sheeran lililofanyika mwezi uliopita na kujaza mashabiki 73,000 ambao waliingia uwanjani.
Pochettino alisema: “Madaktari wanamchunguza na wanaamini jeraha halitakuwa kubwa sana, alianguka vibaya eneo la hatari.
Alihisi maumivu makali kwenye goti lake. Naamini atarudi kabla ya msimu kuanza, tutamuangalia kwa muda wa siku chache ataendeleaje. Nadhani itafahamika tukirudi London.”
Aidha Pochettino alikana kwamba alilalamika baada ya Nkunku kuumia kutokana na uwanja: “Sikulalamika lakini wakati mwingine unatakiwa kuwa makini. Viwanja vingine vinatumiwa kwa michezo mengine au matamasha. Nadhani bahati mbaya na siwezi kuzungumzia vibaya mazingira ya uwanja.”
Nkunku alisajiliwa na Chelsea akitokea RB Leipzig kwa Pauni 53 Milioni ameipa hofu Chelsea kwa sababu imebaki wiki moja tu ligi kuanza na itamenyana na Liverpool.
Tayari Chelsea itakosa huduma ya beki Wesley Fofana ambaye aliumia kabla ya kuanza maandalizi ya msimu kuanza na atakuwa nje ya dimba kwa ilikuwa pigo kubmuda mrefu.
Ilikuwa pigo kubwa kwa Chelsea baada ya Fofana kuumia na ikalazimika kufanya Axel Disasi kutoka Monaco.
Fofana alikuwa na matarajio ya kaunza msimu wa 2023-2024 kwa kishindo baada ya kusuasua msimu uliopita kutokana na majeraha mara kwa mara.
Licha ya Fofana kuumia Chelsea ilifanya uamuzi mgumu wa kuwauza mabeki wake tegemeo wa msimu uliopita Cesar Azpilicueta na Kalidou Koulibaly.
Na kutokana na uhaba wa mabeki ikaingia sokoni kuwinda beki mpya ambaye ataongeza nguvu safu ya ulinzi.