Tukumbushane, leo ni tarehe 25 septemba , siku zikiwa zinaelekea ukingoni mwa mwaka, kwa hesabu za haraka bado miezi mitatu mwaka kuisha kwa mantiki hiyo bado siku 100 kufikia sikukuu ya kuzaliwa Yesu kristu yaani krismasi.

Kama ilivyo mila na desturi zetu katika sikukuu hii familia mara nyingi hupenda kuifanya siku hii kuwa tofauti na siku nyingine, maisha ya siku hii hufanywa kwa utofauti sana kuanzia chakula mavazi hata furaha huwa ni kubwa katika siku hii.

Leo nataka kutoa kaushauri kadogo ambapo kakitiliwa maanani katakuwa na manufaa katika sikukuu hiyo ya krismasi.

Maisha kipindi hiki yamekuwa magumu mnoo, kiasi ambacho sikukuu ikifika inakuwa tu kama siku nyingine za kawaida hatuvai nguo mpya, hatuli pilau, hapo ndipo mzazi hupata hasira maradufu kwa kukosa hela ya siku hiyo ya sikukuu.

Hivyo basi ukitaka siku yako iende vizuri kwako na familia yako kuanzia leo septemba 25, anza kuhifadhi kiasi cha shilingi elfu moja (1000) tu ndani ya siku 100 zilizobaki kufikia krisimasi.

Kwa mahesabu ya haraka hadi kufikia hiyo siku utakuwa umehifadhi shilingi laki moja ambayo hiyo pesa itakusaidia katika kukamilisha shughuli nzima ya chakula kwa hiyo siku na kuwafanya mjisikie tofauti na muifurahie sikukuu hiyo.

 

Wachezaji wamgomea Trump, wapinga vikali agizo lake
Mwendesha Mashtaka Mkuu Kenya aigeukia Tume ya Uchaguzi