Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, kilichopo mkoani Morogoro amewatunuku vyeti wahitimu 142 wa ngazi tofauti chuoni hapo katika mahafali ndogo ya kwanza yaliyofanyika kampasi kuu Morogoro.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka amesema mahafali hayo ni ya kwanza kufanya katikati ya mwaka, lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wahitimu waliokidhi vigezo kupata vyeti na kuvitumia katika sehemu mbalimbali.

Kwa upande wao baadhi wa wahitimu wamesema watatumia elimu waliyopata kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ili kuletewa maendeleo.

Serikali yazindua mpango mkakati wa sekta ya afya
Tundu Lissu auchambua utawala Afrika Mashariki