Chuo Kikuu Huria kimepewa ruhusa ya kuendelea kutoa kozi ya ‘Foundation’ iliyokuwa imesitishwa na serikali kwa wanafunzi ambao wamekosa vigezo vya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu baada ya mtaala wake kuboreshwa na kupitishwa na Wizara ya Elimu.

Ruhusa hiyo imetolewa hii leo mkoani Singida na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipohudhuria katika Mahafali ya chuo hicho.

Aidha, Mwaka 2016 serikali ilitoa agizo la kusitisha kozi hiyo ya ‘Foundation’ kwa kusema kuwa utaratibu huo ulifanywa na vyuo  vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo wa  elimu hiyo.

Bunge lawatosa wabunge CUF
Ujenzi wa machinjio ya kisasa ukamilike kabla ya Desemba- Mpina