Mfanyabiashara wa duka kata ya Chamazi, wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Mateso Chupi (39) amefikishwa mahakama ya wilaya ya Lindi, akikabiliwa na shitaka la kukutwa na vipande sita vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Tsh,67,365,000 visivyo halali.
Chupi amefikishwa kwa Hakimu wa Mahakama ya wilaya hiyo, Mussa Ngaru na kusomewa shitaka linalomkabiri na mwanasheria wa serikali, Abdurahamani Mohamedi.
Mshitakiwa inadaiwa kukamatwa na vipande hivyo vya Meno eneo la kituo cha kuuzia Mafuta mjini Liwale Septemba 27/2008, na kufanikiwa kuwatoroka askari na kwenda kuishi nchi Jirani ya Msumbiji.
“Mh,Hakimu huyu mshitakiwa alikutwa eneo la kituo cha kuuzia Mafuta pale Liwale mjini,akijiandaa kwa safari, lakini kabla ya kuondoka alikamatwa na askari Polisi”Amesema Mohamedi.
Aidha, Mwanasheria huyo amedai kuwa mshitakiwa ambaye hakutakiwa kujibu wala kukataa amefanya kosa chini ya kifungu cha (70) kifungu kidogo cha (1) na (2) na (3) cha Sheria na (283) na kifungu cha (57) cha Sheria ya Uhifadhi wanyama pori namba 5/2009, ikisomwa pamoja na Sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya 2002.
-
Ubadhirifu mkubwa wabainika Shirika la Posta
-
Majaliwa aagiza Wakurugenzi wachunguzwe
-
Serikali yaitahadharisha Simba
Hata hivyo mshitakiwa hakutakiwa kusema lolote, kwani Mahakama hiyo kisheria haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hiyo hadi hapo itakapopata kibari kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).