Ukiwa ndani ya penzi zito na jipya, unakuwa kiziwi na kipofu kwa wapita njia na majirani hata kama wanachokizungumza kina mantiki fulani.

Ciara anaonekana kuwa kimya na kuendelea na maisha yake na boyfriend wake mpya, staa wa NFL, Russell Wilson, ikiwa ni wiki moja baada ya mpenzi wake wa zamani na baba mtoto wake, rapper Future kumtolea maneno makali kwenye vyombo vya habari akiutuhumu uhusiano wake mpya kutomtendea haki mtoto wao.

Chanzo cha karibu cha Ciara kiliiambia E!News kuwa mwimbaji huyo wa ‘Dance Like We Are Making Love’ alichukizwa sana na alichokisema Future lakini hivi sasa ameamua kupotezea.
Ciara na future

“Sasa ana nguvu na furaha. Anafikiri Future anatakiwa kuishi maisha yake na kuuacha uhusiano wake wenye furaha,” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa hata Russel Wilson hana muda na tabia anazozionesha Future.

Future na Ciara waliokuwa wamechumbiana waliachana miezi sita baaada ya kumpata mtoto wao Future Zahir Wilburn.

Hivi karibuni, Future alimtuhumu Ciara kwa madai kuwa amemuingiza mwanaume mwingine kwenye maisha ya mtoto wao kitendo kinachomuathiri mtoto huyo huku wao wakiendelea kula maisha bila kujali.

Wasanii Nane Wa Tanzania Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMMA, Marekani, Diamond Aongoza
Miley Cyrus Atangaza Kusherehesha Tuzo Za Video Za MTV ‘MTVMA’