Kocha wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba amesema wachezaji wake wako tayari kwa mpambano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans utakaochezwa leo Jumatano, Novemba 25 Uwanja wa Azam complex Chamazi.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa moja usiku, unatarajiwa kuwa na upinzani mkali, kufuatia timu hizo kuwa na alama 25 kla mmoja msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza michezo 11.

Kocha Cioaba amesema amefanyia kazi udhaifu uliojitokeza katika mchezo uliyopita ambao walipoteza kwa bao moja dhidi ya KMC FC, hivyo ana uhakika hayawezi kujirudia tena leo watakapoikaribisha Young Africans.

“Wachezaji wangu wote wapo fiti hakuna majeruhi na tupo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Young Africans, utakuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwa sababu wote tunahitaji alama muhimu, kwetu tunazihitaji sana ili kujiimarisha kubaki kileleni na kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya msimu huu,” amesema Cioaba.

Amesema ameimarisha kikosi chake kila idara ikiwamo safu ya ulinzi pamoja na ushambuliaji na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote.

Ubovu wa MV Mapinduzi II wamsikitisha Waziri
Ngorongoro Heroes kuikabili Somalia