Mshambuliaji wa klabu ya Lazio Ciro Immobile amefunga mabao matatu ‘hat-trick’ katika mchezo amabo Lazio imewachapa Ac Millan kwa mabao4-1.

Millan walijikuta hoi katika dimba la Stadio Olimpico huku wakiokota mipira katika nyavu zao mara 3 ndani ya dakika 10 yaliyofungwa na  Ciro Immobile.

Hii ni mara ya kwanza kuona hattrick katika mchezo kati ya Ac Millan na Lazio tangu Andriy Shevchenko kufanya hivyo mwaka 1999 katika dimba la Stadio Olimpique wakati akiifungia Ac Millan mabao matatu .

Immobile sio tu kufunga bao hizo 3 kati ya 4 lakini hata bao la 4 la Lazio ni yeye aliyetoa pasi ya mwisho kwa Luis Alberto aliyefunga bao la nne na kuuacha ukuta wa Ac Millan unaoongozwa na beki kisiki Bonucci kutoamini ni nini kinachowatokea.

Mshambuliaji ameshawahi kuzichezea Juventus akishindwa kufunga bao hata moja, baadae akaifungia Dortmund bao 3 msimu mzima, wakamuuza Sevilla,akapelekwa Torino alikofunga bao 5 na sasa amerudi Lazio.

 

Tutakupa ushirikiano wa kutosha- Ndugai
Nikki wa Pili ataja sababu ya wasanii wengi kutokwenda shule