Klabu ya Leicester City imemteua kocha wa zamani wa Southampon Claude Puel kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Claude Puel anakuwa kocha wa tatu wa klabu hiyo mwaka huu baada ya kutimuliwa kwa Craig Shakespere aliyechukua nafasi Claudio Ranieri ambaye aliiwezesha Leicester City kuchukua ubigwa wa EPL msimu wa 2015/2016 hata hivyo alitimuliwa na klabu hiyo mapema mwezi Februari.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha wa Southampton Puel mwenye umri wa miaka 56 aliiwezesha klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 8 huku pia akiiongoza klabu hiyo kufika fainali ya kombe la EFL ambapo Southampton ailifungwa na Man Utd lakini alitimuliwa ndani ya klabu hoyo.

Puel anachukua kibarua cha kuinoa Leicester City ikiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa imeshinda michezo miwili katika michezo tisa.

Mwenyekiti wa klabu ya Leicester City Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema Puel ndiye chaguo sahihi kwa klabu ya Leicester City.

Afariki kwa kupigwa risasi, wengine 20 wajeruhiwa vibaya
Jaji Warioba awafunda wanasiasa