Meneja wa klabu bingwa nchini England Leicester City Claudio Ranieri amesema kitendo cha klabu hiyo kufanikiwa kumbakiza klabuni Riyad Mahrez, ni dalili  kuwa mambo yatendelea kuwa mazuri licha ya kuanza msimu mpya vibaya.

Leicester City imeanza vibaya kwa kuambulia pointi moja katika michezo yake miwili ya mwanzo ya Premier League, lakini Ranieri anasema kwa kuendelea kuwa na wachezaji kama Mahrez na Jamie Vardy, bado timu hiyo inanafasi ya kutetea taji lake.

Hivi karibuni Riyad Mahrez, 25 alisaini mkataba mpya wa miaka minne na kuzima ndoto za Arsenal iliyokuwa ikiwania saini yake kwa udi na uvumba.

Winga huyo wa kutoka nchini Algeria amefuata nyayo za mshambuliaji Jamie Vary ambaye awali alihusishwa kujiunga na Arsenal kabla ya kuongeza mkataba mpya klabuni hapo.

Msimu uliopita Mahrez aliifungia Leicester City mabao 17 na kutoa pasi za magoli 11 na kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza.

Kabla ya kusaini mkataba mpya, Mahrez alisema ni klabu mbili au tatu duniani ndizo angeweza kujiunga nazo endapo zingemwitaji.

Ummy Mwalimu Azindua Ujenzi wa Jengo La Hospitali Ya Aghakan
Jose Gimenez Amengia Katika Rada Za Arsenal FC