Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton ameahidi kumteua Rais Barack Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo endapo atashinda katika uchaguzi huo.

Bi. Clinton aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mwananchi mmoja katika jimbo la Lowa, aliyetaka kufahamu kama anaweza kumteua Rais Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Mwanasiasa huyo alimsifu muuliza swali na kueleza kuwa amepata wazo ambalo hakuwahi kupewa na mtu yeyote na kwamba ameriridhia kwa kuwa ana nafasi ya kuteuwa majaji watatu wa Mahakama Kuu akiwa Rais.

“Lo! Hilo ni wazo zuri sana. Hakuna mtu amewahi kupendekeza hilo kwangu. Nalipenda sana wazo hilo. Anaweza kuwa na mambo mengine kadha ya kufanya, lakini nakwambia hilo ni wazo zuri sana,” alisema Bi Clinton.

Alimsifu Obama kuwa ni mtu mwelevu na mwenye busara na kwamba alikuwa Profesa wa Sheria hivyo anazo sifa za kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kukichagua chama cha Democratic kwa wingi ili wazo hilo liweze kutimia kwani baada ya kufanya uteuzi, majina ya Majaji wateuliwa huidhinishwa na Bunge la Seneti.

January Makamba: Uchaguzi wa Marudio Zanzibar ni Halali Kikatiba
Justin Bieber ageuka shujaa, amuokoa mwanamke barabarani

Comments

comments