Kocha Msaidizi wa Coastal Union, Fikiri Elias amesema wamekuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu utakaopigwa Mbarali, Mbeya.

Coastal ni miongoni mwa timu ambazo hazijaonja ushindi kwenye ligi na sasa benchi la ufundi limesema kazi itaanzia Mbarali.

Fikiri alikiri kuwa mchezo hautakuwa rahisi kutokana na wapinzani walivyo, lakini kwa maandalizi waliyofanya pamoja na morali iliyopo kikosini watafanya kweli.

Tunaenda kwa tahadhari na umakini kuhakikisha tunashinda mchezo huo ili kujinasua mkiani, tunafahamu ugumu utakavyokuwa ila tutapambana,” alisema kocha huyo.

Tumekuwa na muda mwingi wa maandalizi kuhakikisha tunafanya vizuri.

Matokeo tuliyonayo hayana afya ndani na nje ya uwanja, hivyo lazima tuamke upya.”

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kocha a Ihefu, Moses Basena aliyetambulishwa karibuni kuchukua nafasi ya Zuberi Katwila.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 20, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ajiuzulu