Klabu ya Coastal Union imefungua kesi ya madai dhidi ya Simba, Yanga na Kagera Sugar ikitaka klabu hizo kulipa Sh milioni 75 kwa kuwasajili wachezaji wake kinyume cha sheria.

Coastal inaidai Simba Sh milioni 30 kama fidia kwa kuwasajili wachezaji wake Ibrahim Twaha, Hamadi Hamis na Abdi Banda wakati klabu hiyo iliyoshuka daraja msimu uliopita, ikitaka Yanga kuilipa Sh milioni 20 kwa kumsajili Juma Mahadhi sajili zote zikiwa ni za mwaka 2014/2015.

Pia klabu hiyo yenye maskani yake Tanga inaidai fidia ya Sh milioni 20 klabu ya Mbeya City kwa kuwasajili kinyume cha taratibu wachezaji wake Ayubu Yahaya na Fikiria Bakari huku Kagera Sugar ikidai Sh milioni 5 kwa kumsajili Ibrahim Twaha na kufanya timu hiyo ya Wagosi wa Kaya kuvuna Sh milioni 75 iwapo klabu hizo zitakutwa na hatia kwa kusajili kinyume cha sheria.

Nyota Ya Joe Hart Yazidi Kufifia, Bravo Akaribia Lango La Etihad Stadium
Simba SC Yawasilisha Barua Ya Madai Ya Hassan Kessy