Uongozi wa klabu ya Coastal Union umekanusha taarifa za kufukuzwa kwa kocha wao Juma Mgunda, kama inavyoelezwa katika mitandao ya kijami.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo ya jijini Tanga, Uongozi wa Coastal Union umesiktishwa na taarifa za uzishi za kufukuzwa kwa kocha huyo ambaye kwa kipindi kirefu amekua akikihudumia kikosi chao.

Uongozi wa Coastal Union umewataka Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kupuuza taarifa hizo, na kutambua kuwa, bado unaendelea kufanya kazi na kocha Mgunda kwa mujibu wa mkataba wa pande hizo mbili.

Kisinda aanza mazoezi Young Africans
Mwandembwa kupuliza filimbi Mei 08