Benchi la Ufundi la Coastal Union, limetamba kukiongoza kikosi chao kufanya vizuri katika mechi tatu za mwisho za Ligi Kuu msimu huu na kumaliza katika nafasi nzuri.

Coastal Union imebakiza mechi dhidi ya Ihefu kabla ya kuikaribisha Azam FC na kufunga pazia la ligi kwa kuumana na Simba SC jijini Dar es salaam.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Coastal ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 30 baada ya kúshuka dimbani mara 27.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Fikirini Elius, amesema timu inaendelea na mazoezi ya kujiweka fiti kabla ya kuikabili Ihefu.

Elius amesema pamoja na kutambua ugumu wa michezo ya mwisho ya kufunga pazia la msimu huu, kikosi chake kinatambua umuhimu wa kushinda michezo iliyobaki na kumaliza ligi kwa heshima.

“Mchezo na Ihefu utakuwa mgumu lakini timu inaendelea kujipanga kuikabili na kupata ushindi na kumaliza msimu katika nafasi nzuri,” amesema

Naye Mchezaji wa timu hiyo, Jackson Shiga, amesema anamshukuru Mungu kwa mafanikio ya kikosi chao ambacho kimebaki katika ligi.

“Tunamaliza ligi tukiwa katika nafasi nzuri pamoja na kuwa katika ushindani mkubwa msimu huu, naamini tutamaliza salama na kujipanga kwa msimu ujao,” amesema Shiga

UVCCM waiomba Wizara kuongeza vyuo vya Kilimo
Kompany ajifunga miaka mitano Turf Moor