Mshambuliaji wa Liverpool, Cody Gakpo, anatarajivwa kuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa, baada ya kuumia goti wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur, uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, uliopigwa katika Uwanja wa Tottenham jijini London, Gakpo alitolewa nje dakika 46 na nafasi yake ikichukuliwa na Diogo Jota.

Mholanzi huyo alijiumiza mwenyewe wakati akifunga bao pekee la Liverpool katika mchezo huo ambao timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 2-1.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nchini Uholanzi, Gakpo anaweza kurejea kuitumikia klabu hiyo baada ya mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa mwezi huu.

“Anatarajiwa kuwa nje ya kikosi cha Liverpool kwa wiki kadhaa. Kama mambo yatakwenda vyema, wiki chache (atakosekana),” alisema.

Mwandishi huyo alisema nyota huyo pia, anatarajiwa kukosekana katika michezo ya kikosi cha Uholanzi itakayochezwa mwezi huu.

Alipoulizwa kuhusu jeraha la nyota huyo baada ya mchezo dhidi ya Tottenham, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp. alisema bado hana uhakika wa ukubwa wa jeraha hilo.

“Inawezekana. Sijui. Alivalia kifaa cha kukinga. Alifunga bao lakini baada ya shuti hilo (alilofunga) akajisikia vibaya zaidi,” alisema

Gamondi kusajili wengine Young Africans
Imani Kajula: Tuna imani kubwa na Robertinho