Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la FBI nchini Marekani, James Comey amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote wa karibu anaeweza kubadilisha tabia ya Rais wa Marekani, Donald Trump , amedai kuwa kiongozi huyo hashauriki na tabia zake zinahatarisha hadhi ya nchi.
“Nadhani tabia yake inaathiri hasa hasa kwenye suala la ukweli na jambo la msingi ni jinsi tabia hizo zinavyoathiri taasisi na watu wa karibu wake. Ana tabia ya kuongea uongo na kuwalazimisha wale wanamuunga mkono kukubaliana naye na kuamini”.
Trump alimshutumu Comey kuwa anayoyazungumza ni ya uongo na siasa zake ni za ubaguzi.
Comey alifutwa kazi Mei, 2017 na Rais Donald Trump kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton.
Mbali na Comey kuna idadi kubwa ya viongozi ambao Trump amewafuta kazi kutokana na makosa mbalimbali.