Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi amesema anavunja ushirikiano wa kisiasa baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono-CACH, na vile vilivyo upande wa mtangulizi wake, rais mstaafu Joseph Kabila-FCC.

Amesema hayo wakati akilihutubia taifa hilo jana jumapili ambapo ushirikiano huo umekuwa ukiongoza serikali ya Kongo kwa miaka miwili iliyopita, Kabila akilidhibiti bunge, huku Tshisekedi akiwa na mamlaka ya rais. 

Hotuba yake rais Tshisekedi ilikuwa ikisubiriwa kwa shauku, baada ya mazungumzo ya mashauriano aliyoyafanya mwezi novemba, kwa kile kilichoelezewa kuwa lengo la kuunda muungano wa taifa.

Katika hotuba hiyo, Tshisekedi ameyagusia masuali mengi ambayo amesema yalijitokeza katika mazungumzo hayo, la muhimu zaidi likiwa ni hatua za kuhitimisha ushirikiano baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono yeye, maarufu CACH, na ule wa vyama vilivyo upande wake rais mstaafu Joseph Kabila yaani FCC. 

“Nimeamua kumaliza ushirikiano kati ya FCC na CACH. Hatua hiyo ya kusikitisha imekuja baada ya kujaribu muda wa miaka miwili, kusubiri na kuvumilia ili kuunusuru ushirikiano huo. Miaka miwili ya juhudi ila kwa kweli, hatukufaulu kuepuka hali ya vurugu iliyodumu.” Amesema Rais Tshisekedi.

Ugonjwa wa ajabu waibuka India, 140 walazwa
TAMISEMI yatoa siku 14 kuanza kutumika kwa kituo cha mabasi Mbezi Luis