Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo ya Corona iliyokua ianze leo Jumatatu kwa hofu juu ya usalama wake.

DRC inaungana na baadhi ya nchi za Ulaya kama vile Iceland, Denmark, Norway na Ireland na baadhi kutoka Asia, zilizositisha utoaji wa chanjo hiyo, baada ya baadhi ya watu waliopatiwa kupata athari ya kuganda damu.

DRV imepokea dozi milioni moja na laki saba za chanjo hiyo aina ya AstraZeneca na ilikuwa inatarajiwa kuanza zoezi la kuchanja watu leo, lakini zoezi hilo limeahirishwa kwa kuwa DRC inataka kujiridhisha kwanza na usalama wa chanjo hiyo.

Mpaka sasa chanjo ya AstraZeneca inaendelea ikiwa katika awamu ya tatu ya majaribio na haijathibitishwa na Mamlaka ya chakula na dawa Marekani (FDA).

Mkuu wa Shirika la afya Ulimwenguni (WHO), Tedros Adhanom amenukuliwa akisema chanjo hiyo imeshatolewa kwa watu milioni 335 na hakuna kifo kilichohusishwa na chanjo ya Covid-19, huku wazalishaji wa chanjo hiyo nao wakisema hakuna ushahidi kuwa chanjo hiyo inasababisha kuganda kwa damu.

Djuma avunja ukimya, afunguka kujiunga Simba SC
Wachezaji AS Vita watangaziwa ahadi nzito