Kocha wa Chelsea (The blues), Antonio Conte amesema kuwa baada ya kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya Watford, anaiachia klabu yake kufanya uamuzi kama wanafikiri hafanyi kazi nzuri.
Mabingwa hao watetezi wamepoteza michezo miwili mfululizo ndani ya wiki moja na wako katika nafasi ya nne huku wakiwa na alama 50.
Aidha, Muitaliano huyo alitwaa ubingwa wa ligi katika msimu wake wa kwanza, baada ya kufungwa na Bournemouth na Watford na sasa wako nyuma kwa 19 dhidi ya vinara wa ligi Manchester City.
“Nina fanya kazi na inatosha lakini klabu inaweza kutoa maamuzi mengine kama hawatakuwa wanaridhishwa na utendaji kazi wangu,”amesema Conte
Hata hivyo, Conte amebakiza miezi 18 kabla ya kumaliza mkataba wake, ambapo ameongeza kwa kusema wachezaji wake walicheza huku wakiwa hawana utulivu na kama kocha anabeba msalaba wa lawama.