Hatimaye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limethibitisha kuahirishwa kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani humo hatua ya Makundi kati ya Wydad Athletic Club ya Morocco dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
CAF imetangaza maamuzi hayo baada ya kutokea kwa mkanganyiko wa utoaji wa vibali vya kuingia nchini Morocco ‘VISA’ kwa wachezaji na maafisa wa Kaizer Chiefs, kwa kuhofia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Katika barua ya CAF iliyotumwa Kwa Shirikisho la Soka Afrika Kusini ‘SAFA’, kupitia kwa msimamizi wake wa Idara ya Mashindano, Ahmed Salem alisema ” CAF itawasilisha uamuzi hapo Baadaye”.
Kaizer Chiefs walikuwa wamepanga kuondoka kwenda Casablanca jana Jumatano jioni lakini timu hiyo ilikataliwa visa za kuingia Morocco Sababu ya Virusi vya Corona vilivyochukua nafasi kubwa Afrika Kusini, hatua mabayo iliwalazimu kusitisha safari ya kwenda huko Afrika Kaskazini.
Mchezo kati ya Wydad Athletic Club dhidi ya Kaizer Chiefs ulikua umepangwa kuchezwa Jumamosi (Februari 13) mjini Casablanca, Morocco.