Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limesitisha fainali za mataifa ya bara hilo EURO 2020 ambazo zilipangwa kuanza Juni 12 mpaka Julai 12 mwaka huu.
Kutokana na kikao cha leo, Machi 17, Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin ametangaza kusimamisha msimu huu michuano hiyo mpaka msimu ujao.
Taarifa iliyotolewa Leo na UEFA imeeleza kuwa: “UEFA leo inatangaza kusitisha michuano ya UEFA EURO 2020 kutokana na thamani ya afya za wachezaji na mashabiki kuwa bora kuliko jambo lolote na mpango wetu ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima hii ni kutokana na kusambaa kwa kasi Virusi vya Corona.
CORONA: TFF waitana kwa dharura
“Mechi zote za UEFA na mechi za kirafiki kwa klabu na timu za Taifa kwa Wanawake na Wanaume zinasitishwa mpaka pale tutakapotoa taarifa, mechi zilizotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa zinaweza kuanza mwezi Juni lakini itategemea na hali itakavyokuwa.”
Taarifa ya UEFA imeeleza kuwa fainali EURO zitachezwa mwaka ujao (2021) kuanzia Juni 11 hadi Julai 11.