Hatma ya ligi kuu ya soka nchini England msimu wa 2019/20, itahafamika baadae hii leo, baada ya kikao cha viongozi kutoka klabu 20 zinazoshiriki ligi hiyo.
Kiao hicho kinatarajiwa kuendeshwa kwa njia ya video, lakini taarifa zinaeleza kuwa mamlaka za soka nchini England bado hazijapata mpango sahihi wa namna ya kumalizia msimu huu.
Wakati wakiumiza vichwa, imeripotiwa kuwa moja ya klabu ya EPL, ambayo haijatajwa jina, imependekeza kuwa mechi zilizosalia, zikamaliziwe China, ambako umbali wake ni zaidi ya maili 5,000 kutoka jijini London.
Taarifa za awali zimetanabaisha kwamba, msingi wa pendekezo hilo ni kwamba, lazima mechi zichezwe eneo ambalo angalau kwa sasa liko salama na virusi vya Corona na klabu hiyo imeona China ndio eneo sahihi kwa sababu wamefanikiwa sana kupambana na janga hilo, tangu lilipuke mjini Wuhan mwezi desemba mwaka jana.