Mfanyabiashara tajiri Félicien Kabuga aliyewakwepa waendesha mashtaka wa jopo lililokuwa likichunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa zaidi ya miongo miwili na nusu kwa kutumia majina 28 tofauti ya watu maarufu katika mabara mawili, amekamatwa kipindi hiki cha mlipuko wa corona.
Kulingana na kanali Eric Emaraux, anayeongoza kitengo maalum cha polisi katika kukabiliana na uhalifu, mlipuko wa virusi vya corona ulisadia kwasababu amri ya kutotoka nje ilisitisha operesheni nyingi katika maeneo mengi ya Ulaya, na hivyobasi kutoa fursa ya kumsaka mtu anayedaiwa alikuwa mfadhili mkuu wa mauaji ya kimbari.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 84 amekuwa mafichoni kwa muda mrefu hali ya kwamba jopo la kimataifa lililobuniwa kuchunguza mauaji hayo ya 1994 liliacha kufanya kazi yake.
Lakini hatimaye alisakwa katika maficho yake katika kijiji kimoja cha mji mkuu wa Ufaransa na kupatikana kufuatia uchunguzi ulioanzishwa na Serge Brammerts, mwendesha mashtaka wa Umoja wa mataifa akiongoza jopo linalosimamia uhalifu wa kivita nchini Rwanda na Yugoslavia.
Wachunguzi wa Kimataifa waliwachunguza watoto wake ili kubaini anakoishi baba yao, ambapo alikuwa anaishi kwa kutumia pasipoti kutoka kwenye taifa la Afrika lisilojulikana.
Ikumbukwe kuwa, Katika siku 100 pekee mwaka 1994, takriban watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda na watu wa kabila la Wahutu ambao bwana Kabuga, mfanyabiashara ambaye alikuwa amejinufaisha kupitia sekta ya majani chai aliwaunga mkono.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa MICT, Serge Brammertz amesema kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa jijini Arusha, mahali ambapo Mtuhumiwa alishtakiwa kwa makosa saba mwaka 1997