Mamlaka nchini Italia, zimesitisha ibada katika eneo kubwa la Kaskazini mwa Jiji la Roma kwa lengo la kuzuia kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona.

Jana, Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis aliendesha ibada huko Vatican kwa njia ya mtandao katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo ambao umeshaua watu 366 nchini humo.

Hadi sasa, nchi hiyo inaongoza kwa vifo vingi baada ya china, Idadi imeongezeka kutoka 133 hadi 366. Ongezeko hilo limefanya nchi hiyo kuwa na vifo vingi zaidi nje ya China.

Mbali na kuongezeka kwa vifo, wenye maambukizi ya Virusi hivyo wamefikia 7,375, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25, huku robo ya wananchi wakiwa wamewekwa karantini.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Giuseppe Conte amesema shule, maeneo ya kufanya mazoezi, nyumba za starehe, makumbusho na sehemu nyingine zenye mkusanyiko mkubwa wa watu zitafungwa hadi Aprili 3 mwaka huu.

Ulimwenguni, watu 106,000 wamethibitishwa kuwa na maambukizi huku watu takriban 3,600 wakiwa wamefariki dunia hadi sasa.

Bernard Morrison awashukuru mashabiki
TANROADS yafunga daraja Mwanza