Kufuatia maagizo ya Rais wa Kenya ya watu kufanya kazi nyumbani ili kuepusha virusi vya Covid 19 kuendelea kuenea nchini humo, karani mmoja wa benki ametumia mwanya huo kuiba pesa.
Karani huyo wa benki amekamatwa kwa kujaribu kubeba zaidi ya Ksh 800,000 kwa kisingizio kwamba alikuwa akipanga kufanyia kazi nyumbani.
Imeelezwa kuwa alichukua fedha hizo na kujaribu kuondoka nazo wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana ambapo walinzi walitaka kujua yaliyomo kwenye ‘briefcase’ kabla ya kumruhusu na alisema ameruhusiwa kufanyia kazi nyumbani kwa kuwa alikuwa akikohoa.
CORONA: Idadi ya vifo Italia yazidi China, 427 wafariki kwa siku
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa mbioni kupanda basi kutokana na kuonekana kwenye video za CCTV akiwa amebeba vifurushi 160 vya bahasha zilizo na noti.