Kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI, Condom inatarajiwa kuwa adimu Duniani kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona kusababisha viwanda kufungwa huku Umoja wa mataifa UN ukionyesha hali hiyo inaweza ikaonyesha matokeo mabaya zaidi.
Kwa mujibu wa AFP, Mtendaji mkuu wa kiwanda cha Karex Goh MIah KIat amesema wazalishaji wengi duniani wanakabiliwa na uwezekano wa kuvurugwa kwa shughuli zao na ugumu wa kusafirisha condom hadi sokoni.
”Ni dhahiri dunia itakumbana na upungufu wa condom, nichangamoto lakini tunajaribu kila tuwezalo, ni dhahiri inatia wasiwasi condomu ni zana muhimu katika tiba” amesema Goh MIah KIat.
Kutokana na mazuio yaliyowekwa dhidi ya kiwanda kikubwa cha uzalishaji wakinga cha Karex ambacho huzalisha condom moja kati ya tano zinazopatikana duniani kote, kiwanda hicho kitatoa codom millioni 200 pungufu ya uzalishaji wa kawaida kuanzia mwezi machi hadi April.
Hayo yamejiri kwakuwa idadi kubwa ya watu duniani imejifungia majumbani wakati huu wa ugonjwa wa covid 19 ambao unaambukiza kwa kasi huku serikali zikiagiza kufanga kwa biashara zinazoonekana kutokuwa na umuhimu.
Malaysia moja kati ya nchi inayozalisha mpira kwa wingi duniani iliyopo Asia kusini mashariki na mzalishaji wa Condom, ilitangaza marufuku ya kutotoka nje kwa nchi nzima wakati maambukizi yakifikia kiwango cha juu katika taifa hilo.